Ungozi wa klabu ya Yanga umesema hauna tatizo na golikipa Juma Kaseja endapo atataka kujiunga na timu nyingine yoyote ambayo ipo tayari kumsajili kwa ajili ya kuitumikia kwasababu kwa sasa mchezaji huyo hayupo kwenye orodha ya wachezaji wa klabu hiyo kwasababu mchezaji huyo tayari alishavunja mkataba wake na Yanga.
Mwanasheria wa klabu ya Yanga Frank Chacha amesema, Kaseja si mchezaji wa Yanga kwasababu alijitoa mwenyewe kwa kuandika barua ya kuomba kuvunja mkataba na klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani kwa madai kwamba hakulipwa pesa yake ya usajili.
Chacha amefafanua kuwa, wachezaji wa mpira ni waajiriwa kama waajiriwa wenine ndio maana Kaseja na Jaja wameshtakiwa kwenye mahakama ya kazi ya ndani na sio mhakama nyingine. Chacha aliendelea kusema kuwa, kwakuwa Kaseja alikuwa ni mwajiriwa wa Yanga na ameamua kuacha kazi mwenyewe, kesi ya madai dhidi yake haimzuii yeye kuendelea kucheza mpira na kama anataka kusajiliwa kwenye timu nyingine yuko huru kufanya hivyo.
Wanachokitaka Yanga kutoka kwa Kaseja ni madai yao ya kuvunja mkataba, Yanga imeshazungumza na golikipa huyo pamoja na wakili wake kwamba akitaka barua ya kuondoka Yanga ‘release letter’ wao wako tayari kumpatia lakini suala la kesi litabaki palepale.
Kaseja alishtakiwa na klabu ya Yanga kwenye mahakama ya kazi ambapo kesi hiyo bado inaendelea, Madai ya Yanga ni kwamba baada ya Kaseja kuvunja mkataba wao wanataka awalipe fidia ya kuvunja mkataba kwasababu tayari walishampatia kiasi cha fedha kwa ajili ya usajili wake.
Hapa chini nimekuwekea stori nzima ya mwanasheia wa Yanga akifafanua kwa kina jambo hilo, bofya hapo kuisikiliza;