Klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza imeamua kumfungia kazi mshambuliaji Fernando Llorente wa Juventus ya Italia katika dirisha hili kubwa la usajili.
Imeelezwa kuwa Liverpool imefikia uamuzi huo baada ya kutokubaliana na dau la mshambuliaji wa Aston Villa, Christian Benteke anayeuzwa kwa dau la paundi 32.5m.
Liverpool imeona dau hilo ni kubwa kwa Benteke na kwamba wameamua kuwafuatilia Fernando Llorente pamoja na mshambuliaji wa mabingwa wa Uropa klabu ya Sevilla ya Hispania, Carlos Bacca.
Ingawa Carlos Bacca ana kipengele kinachomfanya kuuzwa kwa dau lisilopungua paundi 21m lakini Liverpool inaona ni heri zaidi ya dau hilo la Benteke.
Llorente mwenye miaka 30 hivi sasa amekua sio mchezaji muhimu katika kikosi hicho cha mabingwa wa Italia msimu huu na kwamba inaweza kuwa rahisi zaidi kwa Liverpool kumpata kutokana pia Juventus pia wamewasajili Mario Mandzukic pamoja na Dybala huku kijana kutoka Hispania, Morata naye akiwa kikosini.
Inasemekana kuwa kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anahitaji uzoefu katika chumba cha kubadilishia nguo kutokana na kuwa na idadi kubwa ya vijana wenye umri mdogo.
Tayari Liverpool imewasajili James Milner, Adam Bodgan na Dany Ings huku ikimnasa pia chipukizi anayecheza England U19 Joe Gomez.
Klabu hiyo iko busy kurudi inakostahili baada ya kufanya msimu huu vibaya tofauti na matarajio baada ya kumkosa Luis Suarez waliyemuuza Barcelona pamoja na majeruha ya mara kwa mara ya Daniel Sturridge ambao waliingoza timu hiyo kufanya vizuri misimu miwili iliyopita.
Ikumbukwe kuwa msimu ujao itakua ni mara ya kwanza kwa Liverpool ndani ya karne hii kucheza bila nahodha wao wa muda mrefu, Steven Gerrard anayetimkia Los Angeles Galaxy Marekani.