Didier Drogba mchezaji mwenye heshima kubwa katika soka la Africa na Ulaya anaendeleza kuonyesha jinsi gani heshima yake ni kubwa sana kwenye jamii ya wapenda soka.
Kitu kilichotokea ni kwamba Salomon Kalou aliandaa tukio la kujitolea ili kuchangisha pesa ambazo ni sehemu ya michango ya mfuko wa Salmon Kalou Foundation ambazo zinatumika kwenye project mbalimbali.
Kwenye tukio hilo Drogba aliuza jezi yake kwenye mnada wa kuchangia na ilifanikiw kuuzwa kwa kiasi cha millioni 15. Lakini pia wachezaji wengine ambao waliuza jezi zao ni kama Yaya Toure ambapo yake iliuzwa kwa $3500 na Gervinho yake imeuzwa kwa $850.
Kalou yeye mwenyewe alitoa kiasi cha $25000 kwa ajili ya Foundation yake na Drogba binafsi alichangia pesa za kununua mashine kwa ajili ya hospitali inayosimamiwa na Foundation hiyo ambapo mashine hiyo ina gharama ya $50000.