Juventus midfielder Arturo Vidal amemwaga machozi akiwa anaomba msamaha baada ya kupata ajali akiwa anatoka kwenye starehe za usiku na mke wake.
Vidal ambae alisababisha ajali akiwa na mke wake kwenye gali wakitokea casino aligonga gari lake la kifahari aina ya Ferrari na kusababisha ajali kwa watu wengine waliokua maneo hayo na magari yao.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari Vidal alitokwa na machozi akielezea jinsi gani anajisikia vibaya baada ya kuhatarisha maisha ya mke wake kwenye ajali hiyo.
Vidal alisema alienda Casino na kupata glass mbili za kinywaji ambacho hakukitaja na kuanza safari ya kuelekea nyumbani na njiani ndio mambo yote hayo yalitokea.
Vidal alisema ningependa kuomba msamaha kwa kila mtu na watu waliohusika kwenye ile ajali. Nitafanya kila niwezalo uwanjani kuisaidia nchi yangu ya Chile kufanya vizuri kwenye Copa America.
Vidal ameruhusiwa kuendelea na michuano ya Copa America pamoja na wenzake.